Kamati ya Huduma ya Mikopo ya Halmashauri ya Wilaya ya Chato ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg.Geriad Mgoba leo Oktoba 1,2025 imefanya ziara ya kukagua jumla ya Vikundi 62 vya Wanawake,Vijana na watu wenye Ulemavu kutoka Kata 23 vilivyoomba kupewa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri hiyo.
Katika ukaguzi huo kamati imetembelea Vikundi kwenye maeneo yao ya biashara na kuhakiki biashara wanazofanya na mazingira na namna wanavyoendesha biashara hizo. Mwenyekiti wa kamati amevisisitiza Vikundi vyote vilivyo kaguliwa kuhakikisha vinafata ushauri wa kitalaamu kutoka kwa wataalamu wa halmashauri ili kufanya biashara zao kwa Ufanisi na kuzalisha kwa wingi kuepukana na Hasara.
“Ninaomba mzingatie sana ushauri na kanuni za kitaalamu za biashara husika mnazofanya,kama ni kilimo mfuate ushauri kwa maafisa kilimo,kama ni ufugaji pia wapo wataalamu wetu wa mifugo watawaelekeza namna sahihi ya kufuga ili fedha hizi mnazoomba kupewa,mzifanyie kazi kwa kwa usahihi na kuzalisha faida ili mrejeshe kwa wakati” Ndg. Mgoba.
Mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Chato kwa awamu ya kwanza ya mwaka wa fedha 2025/2026 inatarajiwa kuanza kutolewa mnamo mwezi Novemba 2025.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.