Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chato Mkoani Geita Ndg. Mandia H. Kihiyo mapema hii leo ameongozana na Kamati ya Wataalamu katika ukaguzi wa Miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya wilaya ikiwa ni katika kuhakikisha Miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa kuzingatia Ubora na thamani ya fedha iliyotolewa.
Aidha amewataka watumishi wote waliopewa jukumu la kusimamia utekelezaji wa Miradi hiyo kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya ubadhirifu katika kusimamia miradi hiyo ikiwa ni pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu za manunuzi katika kila hatua ya utekelezaji wa miradi hiyo ya Maendeleo katika maeneo yao.
MKURUGENZI MTENDAJI
Postal Address: 116 CHATO
Telephone: +255282228007
Mobile:
Barua pepe: ded@chatodc.go.tz
Copyright©2016 CDC . All rights reserved.